Daftari La Utetezi Wa Imani Kwa Wachungaji Na Watumishi Wa Kikristo

Transcription

Daftari la Uteteziwa Imanikwa Wachungajina Watumishiwa KikristoPima kabla hujaamini!1 Wathesalonike 5:21–22Kumbuka Hatua TatuPIMAKila KituZINGATIAkilicho ChemaEPUKAKila Aina ya Uovu

Kuhusu “The Africa Centre for Apologetics Research”(ACFAR, au Kituo cha Uchunguzi wa Utetezi wa Imani Afrika)Dhamana ya ACFAR imejengwa katika Agizo Kuu la Yesu katika Mathayo28, akituagiza kufanya mataifa yote yawe wanafunzi wake. Uanafunzi wakibiblia unahusu kuwakuza waumini wapate kukomaa kiroho na kuwa naumoja, na katika hili, lazima tuufuate mfano wa mitume.Msisitizo wetu ni wenye sehemu tatu:Kwanza, tumepewa jukumu la kuwatayarisha watu wa Mungu wawe na uwezo wakupambanua, yaani, kuwasaidia kutofautisha kimaandiko kati ya ukweli na uongo,wema na ubaya, mwanga na giza. Tunajitahidi kuwapa uwezo wa kutambua utofauti wadhati “kati ya kilicho sahihi na kinachokaribia kuwa sahihi,” utofauti ambao makanisa yauongo na walimu wa uongo huutumia. Makanisa na walimu bandia hustawi pasipokuwepowatu “waliokomaa, waliofunzwa kwa vitendo kubainisha mema na mabaya”(Waebrania 5:14).Pili, tunalenga kuwafundisha waumini kwa ajili ya ulinzi waimani “waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yuda 3–4).Agizo hili linatulazimu sisi kuishindania imani kwa nguvu katikauso wa upinzani. Si kwa silaha za kibinadamu za kuangamiza,bali kwa kiasi, kwa ukweli, kwa unyenyekevu tunapaswa kusemaukweli ambao Mungu amefunua kwa Roho wake katika MaandikoMatakatifu. Tito 1 hasa inawalazimu wachungaji, ambao ni mstariwa mbele wa ulinzi dhidi ya uongo, washike “kikamilifu ujumbe ule wa kuaminika kamaunavyofundishwa. Ndivyo watakavyoweza kuwatia wengine moyo kwa mafundisho sahihi nakuyafichua makosa ya wale wanaopinga mafundisho hayo.”Tatu, tunalenga kuwahamasisha Wakristo wapate kufanya uinjilisti kati ya walewaliodanganywa na makanisa ya uongo, jukumu ambalo ni muhimu lakinilimezembewa. Ina maana kwamba kuwasaidia kwa upendo wanaume, wanawake, na watotowalionaswa katika makanisa ya uongo, wamwamini Yesu Kristo kama Mungu hai na wa kweli,na kushika tumaini ambalo yeye tu anaweza kuwapa.Siku hizi, Wakristo wanalengwa na makanisa na walimu wa uongowanaokusudia kuwadanganya, kuwapotosha, na kuharibu imani yao.Waumini wengi sana, hata wachungaji, hawajatayarishwa kupambana na hili. ACFAR inawafundishawachungaji na watumishi wengine wa Kristo kufahamu na kutumia ukweli wa kibiblia ili wawezekuwajibika ipasavyo dhidi ya mkanganyiko wa kiroho na upinzani unaotuzunguka.Kwa neema ya Mungu, tunafanya kazi hii kupitia uchunguzikuhusu makanisa ya uongo, kupitia huduma ya redio, na kwakuandika na kusambaza maarifa kwa machapisho na kwenyemtandao kuikabili kiu iliyoenea ya kupata majibu. Kazi hiiinawezeshwa kwa ushirikiano na makanisa, huduma zingineza kikristo zenye mtazamo mmoja, na watu waaminifu.Tunatumaini kwamba utaomba pamoja nasi na pia kwa ajili yetu, na kutuunga mkono tukilenga kutimizamwito wa Agizo Kuu kwa kuwafanya watu wawe wanafunzi wa Yesu na si wanaojiita wakristo tu, na hivyowawe wakristo wenye ujasiri na uwezo wa kupima kila kitu, kuzingatia kilicho chema, na kuepuka kila ainaya uovu (1 Wathesalonike 5:21–22).

Wewe na Utetezi wa ImaniKatika kiingereza neno apologetics(au, utetezi wa imani) limetoholewakutoka neno la Kigriki apologia (au,ulinzi). Utetezi wa imani, kazi inayokaziaulinzi wa Ukristo, ni jukumu ambalolinaonekana kupotea katika kanisala sasa. Siku hizi msisitizo mkubwaunaonekana kuwa kitu kama hiki,“Mungu ni Mungu wa upendo. Hebu,tupendane. Tusikabiliane na imaniza watu wengine, kwa sababu huo siupendo.” Lakini, tofauti na mawazokama haya, Yesu (ambaye ni kielelezocha upendo) alikabili kwa nguvu imaniza watu alizokutana nazo (k.m. Mathayo23). Lazima sisi tuufuate mfano wake.Utetezi wa Imanihuthibitisha kwanini tunaamini kiletunachoamini.Maandiko yametupa sisi mifano yakufanya utetezi wa imani. Mtume Paulo,kwa mfano, alifanya kazi ya mteteziwa imani alipotoa sababu za kuaminikwa Wayahudi na kwa watu wa mataifa(Matendo 17:15–34; 18:4). Apolo nimfano mwingine mzuri sana, kwanikatika Akaya aliitetea imani kwa dhati,akiwashida wapotevukatika majadilianoya hadharani nakuthibitisha kutokakwenye Maandiko kwamba Yesuni Kristo (Matendo 18:24–28).Utetezi wa imani huwapa wapotevusababu za msingi zinazowawezeshawachague Ukristo badala ya dini yoyotenyingine. Utetezi wa imani unawezakutumika kumwonyesha mpotevukwamba chaguzi za dini zote zinginekikweli si chaguzi sahihi, kwani niza uongo. Utetezi wa imani unawezakuondoa vikwazo vya kimawazo vizuiavyowapotevu ili wapate kuipokea injili.Utetezi wa imani si kwa ajili yakuwathibitishia wapotevu tu, bali pia nikuwapa Wakristo usalama wa kiroho.Waumini wanaweza kuwa na uhakika wakwamba imani yao si bila msingi, bali niuchaguzi wenye busara uliojengwa juu yaukweli. Utetezi wa imani haubadili imaniyetu, bali unaimarisha imani tuliyo nayo.Haya yameandaliwa kutokana na 5-Minute Apologeticsfor Today copyright 2010 na Ron Rhodes Ilichapishwa na Harvest House Publishers, Eugene, OR97402 USA www.harvesthousepublishers.com Hayayametumika kwa ruhusa ya mwandishi.Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,na kufanya uinjilisti kati ya washiriki wa makanisa ya uongo.www.ACFAR.org barua pepe info@ACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664

Dini Zote si SawaWatu wengine wanadai kwamba dini zote kwa ujumla ni sawa, na tofautizilizopo ni ndogo sana. Ukweli ni kwamba tofauti zilizopo kati ya dini zoteni za msingi na si za juujuu tu.Watu wengine husema kwamba dini zote zinafanana kwa sababu zote zinafundishamaadili. Ukweli ni kwamba dini zote zingine za dunia zinalenga kuwasaida watuwabaya wapate kuwa bora zaidi kwa kuchagua maadili ya kibinafsi yaliyo bora zaidi.Kwa upande mwingine, Ukristo huwaalika watu waliokufa kiroho kuwa hai kiroho(Yohane 3:5).Hili linafanikishwa kupitiasadaka iliyo kifo cha Yesu(2 Wakorintho 5:21). Yesualidai kwamba manenoyake yana kipaumbelekuliko mafundisho yawatu wote wengine. Alisemakwamba yeye ni njia ya pekee ya wokovu kwabinadamu (Yohane 14:6). Wale waliomfuatawalithibitisha hili (Matendo 4:12; 1 Timotheo2:5). Yesu pia alionya kuhusu watu wengineambao wangedai Kristo tofauti (Mathayo24:4–5).Mtu akidaikwamba dinizote ni sawa,anaonyeshakwambaDini mbalimbali pia zinafundisha mitazamotofauti kuhusu Mungu. Yesu alifundishakuhusu Mungu aliye Utatu (Mathayo28:19). Muhammad, mwasisi wa Uislamu,alifundisha kwamba yule Mungu mmoja sialiye Utatu. Dini ya kihindi inaamini miungumingi ambayo ni sehemu ya mungu mmojaaitwaye Brahman ambaye hana utu (yaani ni“impersonal”). Ubudha unafundisha kwamba dhanakuhusu Mungu kweli haina maana. Kama dini moja ya hizini sahihi, zile zote zingine si sahihi. Kama Yesu alikuwa sahihi, kamawanavyoamini Wakristo, zote zingine si sahihi.hazielewi dinihizo.Haya yameandaliwa kutokana na 5-Minute Apologetics for Today copyright 2010 na Ron Rhodes Ilichapishwana Harvest House Publishers, Eugene, OR 97402 USA www.harvesthousepublishers.com Haya yametumika kwaruhusa ya mwandishi.

Wakristo Wanaweza KudanganywaNi muhimu kuutafuta ukweli,kujiuliza maswali, na kufikiri kwakina kwa sababu Wakristo wanawezakudanganywa, yaani, wanawezakukubali mafundisho yasiyo sahihi.Ezekieli 34:1–7 husema wazi kwambawanakondoo wa Mungu wanawezakudhulumiwa na kupotoshwa nawachungaji waovu. Aidha, Yesualiwaonya wafuasi wake kuchukuatahadhari dhidi ya manabii wa uongowanaoonekana kwa nje kuwa wemalakini kwa ndani ni hatari (Mathayo7:15–16). Kwa nini Yesu aliwaonyawafuasi wake kama haiwezekanikudanganywa?Wakristo wasioimarishwakatika ukweli wa kibibliandio hasa walio hatarinikukubali mafundisho yauongo. Kwa hiyo, wakristowanahitaji kujijengakabisa kiroho katikaMaandiko kila siku.Yesu pia alionya wafuasi wake,“Jihadharini msije mkadanganywana mtu. Maana wengi watatokeawakisema kila mmoja kwamba yeyendiye Kristo nao watawapotosha watuwengi .Watatokea manabii wengiwa uongo watakaowapotosha watuwengi” (Mathayo 24:4, 11). Kwa niniYesu anawaonya wafuasi wake kuhusuudanganyifu kama wasingewezakudanganywa na, mwisho wake,kuuamini uongo?Hali kadhalika, katika 2 Wakorintho11:2–3, mtume Paulo aliwaonyaWakristo katika mji wa Korintho kuhusuuwezekano wa kuacha uaminifu wakweli kwa Kristo na kupotoshwa namafundisho ya uongo.Katika Matendo 20:28–30, Pauloaliwaonya wazee katika Efeso kuwamacho na kuchukua tahadhari kuhusukanisa, hasa dhidi ya walimu wauongo wasemao “mambo ya uongoili kuwapotosha watu na kuwafanyawawafuate wao tu” (Angalia pia Waefeso4:14; 2 Timotheo 4:3–4).Haya yameandaliwa kutokana na 5-Minute Apologeticsfor Today copyright 2010 na Ron Rhodes Ilichapishwa na Harvest House Publishers, Eugene, OR97402 USA www.harvesthousepublishers.com Hayayametumika kwa ruhusa ya mwandishi.Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,na kufanya uinjilisti kati ya washiriki wa makanisa ya uongo.www.ACFAR.org barua pepe info@ACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664

Manabii na Walimu wa UongoMara nyingi, Maandiko yanaonyadhidi ya manabii wa uongo nawalimu wa uongo kwa sababu watuwa Mungu mwenyewe wanawezakudanganywa (Ezekieli 34:1–7;Mathayo 7:15–16, 24:4, 11). Kwahiyo, Biblia huwahimiza wauminikuwapima wale wanaojidai kuwamanabii (Angalia 1 Yohane 4:1–3).Kwa namna gani wauminiwanaweza kumtambua nabiiwa uongo? Fikiria mawazohaya ya msingi:Manabii wa uongo wanatabirikisichotimia. (Kumbukumbu 18:21–22).Manabii wa uongo nyakati zinginewatawashawishi watu kufuata miunguya uongo na sanamu (Kutoka 20:3–4;Kumbukumbu 13:1–3).Manabii wa uongo mara nyingihukana uungu wa kweli wa Yesu Kristo(Wakolosai 2:8–9).Tunapaswa kufuata mfanowa Waberea kwa kupima naMaandiko mafundishoyoyote yanayodaiwakuwa kweli.(Matendo 17:11;1 Wathesalonike 5:21)Manabii wa uongo mara zinginewatakana ubinadamu wa Yesu Kristo(1 Yohane 4:1–2).Manabii wa uongo mara zinginehuagiza kuepukana na vyakula fulanikwa sababu za kiroho (1 Timotheo 4:3–4).Manabii wa uongo mara kwa marahuhimiza masharti mengi (Wakolosai2:16–23).Manabii wa uongo mara zinginehufundisha kwamba ndoa ni kitukibaya (1 Timotheo 4:3).Manabii wa uongo mara kwa marahupendekeza aina mbalimbali za uzinzi(Yuda 4–7)Kama mtu anayesemekana kuwa nabiiakisema chochote ambacho kinapingasehemu yoyote ya Neno la Mungu,mafundisho yake yasikubaliwe. Nenola Mungu ni kipimo cha ukweli, kipimokinachobainisha uongo.Haya yameandaliwa kutokana na 5-Minute Apologeticsfor Today copyright 2010 na Ron Rhodes Ilichapishwa na Harvest House Publishers, Eugene, OR97402 USA www.harvesthousepublishers.com Hayayametumika kwa ruhusa ya mwandishi.

Mafundisho ya Lazima ya Imani ya KikristoMafundisho ya msingi ya Biblia yamekuwa ni kiini cha Ukristokwa miaka 2,000. Kwa ujumla, Wakristo wote wanaotaka kuwana imani iliyo ya kibiblia wanayakubali mafundisho haya.Labda Wakristo hawakubaliani kuhusu mafundisho madogomadogo katika imani, lakini wanapaswa kukubaliana kuhusumafundisho makuu, kweli hizi zilizo kiini cha Ukristo.Tunaweza kutambua mafundisho ya kimsingi ya imani ya kikristo kwakuchunguza ukweli wa Injili, ulio wokovu wa binadamu kupitia maisha,kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo. Wokovu, kama Mungu alivyokuwa ametufunuliakatika Maandiko Matakatifu yake, unamaanisha kwamba msamaha wa dhambina uhai wa milele na Mungu unapatikana kwa kukiri kwamba “Yesu ni Bwana” nakuamini kwamba Mungu alimfufua Yesu kutoka wafu (Waroma 10:9). Tukichunguzaujumbe wa Injili, tunaweza kutambua mafundisho kumi na nne (14) ambayo ni yalazima ili kupata wokovu kuwezekane.Mafundisho ya kimsingi ya Ukristo yahusu: Mungu ni nani Yesu Kristo ni nani Upendo wa Mungu kwa watu, na hamu yake kuwaokoaHaya ni mafundisho 14 ya kimsingi kuhusu wokovu ambayo lazima yawe ya kweliau mtu yeyote hawezi kumjua Mungu na kuokolewa:1 Umoja wa MunguKuna Mungu mmoja tu aliye wa kweli. Tangu milele ya zamani yupo, na atakuwepokwa milele ijayo. Kuna Mungu mmoja, mmoja tu, aliye Muumba wa vyote.2 Utatu wa MunguIngawa kuna Mungu mmoja tu, yupo tangu milele ya zamani akiwa na nafsi tatu:Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.3 Upotovu wa Binadamu WoteMungu anataka kujulikana na watu na kuwa na mahusiano na binadamu. “Upotovuwa binadamu wote” unamaanisha kwamba kila mtu ametengwa na Mungu kiroho,na hana uwezo kabisa wa kujiokoa.UKURASA WA 1 2 3Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,na kufanya uinjilisti kati ya washiriki wa makanisa ya uongo.www.ACFAR.org barua pepe info@ACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664

Mafundisho ya Lazima ya Imani ya Kikristo4 Kristo Kuzaliwa na BikiraYesu alizaliwa kwa njia ya ajabu, kwa njia ya muujiza wa Mungu: Maria, mama yakeYesu, alipata mimba bila kukutana na mume au kujuana kimwili.5 Kristo Kutotenda Dhambi KabisaKristo alizaliwa na bikira, hivyo ubinadamu wake haukuathiriwa na dhambi. Kwamaisha yake yote Yesu hakutenda dhambi.6 Uungu wa KristoKulikuwa na njia moja tu ya binadamu kupatanishwa kiroho na Mungu. Mungu, bilakuacha uungu wake kwa kiasi chochote, alijivika na ubinadamu wetu, akawa mtumkamilifu katika Kristo. Kristo asingekuwa Mungu na binadamu kwa mara moja,asingeweza kuwa mpatanishi kati ya Mungu na binadamu (1 Timotheo 2:5).7 Ubinadamu wa KristoIngawa Yesu ni Mungu, pia yeye ni binadamu kabisa. Yesu aliwahi kuchoka;Alisinzia; Alitoa jasho; Aliwahi kuwa na kiu na njaa. Yesu asipokuwa binadamuasilimia mia, asingeweza kutoa malipo ya dhambi za binadamu. Alihitaji kuwana uungu ili awe na uwezo wa kutuokoa, na alihitaji kuwa na ubinadamu ili apatekutuwakilisha sisi binadamu. Lazima Kristo awe Mungu na Binadamu.8 Ulazima wa Neema ya MunguKwa sababu ya upotovu wa binadamu, hatuwezi kujiokoa. Ni kwa njia ya neemaya Mungu tu kwamba wokovu unawezekana. Mungu ana haki ya kuwawajibishabinadamu kwa sababu ya dhambi zao. Lakini, kwa neema yake, watu wasiostahiliwatapata ushirikiano naye na kuepukana na hukumu. Bila neema ya Mungu, hakunamtu yeyote ambaye angaliweza kuwa na uhusiano na Mungu.9 Ulazima wa ImaniImani ni kutegemea kwamba Mungu anaweza kutuokoa na atatuokoa. Hakuna mtuyeyote anayeweza kustahili wokovu. Hakuna kiasi chochote cha matendo memaambacho kinaweza kumrudishia Mungu deni analodai. Lakini, kwa kumwaminiMungu na kwa kupokea kwa shukrani zawadi yake ya wokovu, tunaweza kupatananaye Mungu. Kuamini ni wajibu wetu, lakini si tendo linalotustahilisha. Kuamini nikumtegemea Mungu afanye kile ambacho tusingeweza kukifanya wenyewe (Waefeso2:8–9; Tito 3:5–6).10 Kifo cha Kristo kuwa Malipo ya DhambiHukumu ya dhambi ni kifo—na si kifo cha kimwili tu (kilicho utengano kati ya rohozetu na miili yetu), bali pia ni kifo cha kiroho (kilicho utengano kati yetu na Mungu).Malipo anayotudai Mungu yalilipwa na Kristo kupitia kifo chake msalabani. Malipoyaliyofaa yalihitaji kuwa makamilifu, bila kasoro au upungufu. Kristo, aliye mtumkamilifu, alijitoa kwa niaba yetu, ili kwamba kila amwaminiye hatakufa (kimwili aukiroho) bali atakuwa na uhai wa milele (Yohane 3:16).UKURASA WA 1 2 3

Mafundisho ya Lazima ya Imani ya Kikristo11 Ufufuo wa Kristo KimwiliKifo cha Yesu kilikuwa malipo ya dhambi zetu, lakini mchakato wa kutupatiawokovu haukuisha mpaka alipokishinda kifo kwa kufufuka kimwili katika mwiliuleule (Yohane 2:19–21). Kwa sababu Kristo ni mshindi dhidi ya kifo na mwili wakeni mfano wa miili ya ufufuo, binadamu wote watafufuliwa na kuishi kwa milelembinguni au kwenye ziwa la moto.12 Kristo Kupaa Kimwili Kwenda MbinguniKristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka kimwili kwa ajili ya wokovu wetu.Baada ya siku arobaini, alipaa kimwili kwenda mbinguni.13 Upatanisho wa KristoKupaa kwa Kristo kimwili kulimwezesha awe mpatanishi wetu (au kuhani mkuu)mbele za Mungu. Mbele zake Mungu, Kristo hutuombea daima.14 Ujio wa Pili wa YesuKama vile alivyoondoka toka duniani kimwili, ndivyo atakavyorudi. Ujio wa pili waYesu ni tumaini la dunia. Atakaporudi, waumini wafu watapata miili yao ya ufufuo.Waumini walio hai atakaporudi, hawatakufa, bali miili yao itabadilishwa kuwamiili itakayodumu kwa milele. Ujio wa Kristo wa kimwili utaonekana kwa wote, nawaumini watatawala pamoja naye katika ufalme wake na kuishi pamoja naye kwamilele. Wale wasioamini watatengana na wema wake Mungu milele.Kuamini au Kutoamini?Si lazima mtu aelewe mafundisho haya yote wakati anapomwamini Yesu na kuokolewa.Kuna utofauti kati ya mafundisho yale ambayo ni lazima yawe kweli ili tuokolewe namafundisho yale ambayo ni lazima tuamini ili tuokolewe. Kwa mfano, hakuna sehemuyoyote katika Biblia ambayo inasema ni lazima kuelewa kwamba Yesu alizaliwa nabikira ili kwenda mbinguni; hata hivyo, ukweli wa kwamba Yesu alizaliwa na bikiraunatuhakikishia kwamba Mungu alifanya kazi katika kuvunja minyororo ya dhambikupitia Mwanae Yesu.Kuna mafundisho mengine ya lazima ambayo labda mtu hayajui wala hayaelewi moja kwamoja lakini bado ameokolewa (kama ukweli wa kwamba Yesu alizaliwa na bikira, alipaakwenda mbinguni, na atarudi duniani tena). Kusema hivi si kuleta maana ya kwamba mtuanaweza kuyakana (akiyasikia) na bado kuokolewa, bali ni kusema hahitaji kuyaelewamoja kwa moja ili aokolewe. Aidha, kuna mafundisho mengine ya lazima ambayo ni lazimakuyaelewa hapohapo ili kuokolewa. Mtu lazima aamini kwamba Kristo alikufa kwa ajiliyetu, akafufuka (Waroma 10:9; 1 Wakorintho 15:1–6). Mtu lazima aamini “katika BwanaYesu Kristo” (Matendo 16:31). Neno “Bwana” (kurios katika Kigiriki) likimrejea Kristokatika Agano Jipya linamaanisha “aliye Mungu,” kwa hiyo mtu hawezi kukana uungu waKristo na kuokolewa (Matendo 2:21, 36; 3:14–16; 5:30–35; 10:39; 1 Wakorintho 12:3).Haya yameandaliwa kutokana na Essential Doctrine Made Easy na Norman L. Geisler (Rose Publishing, 2007)UKURASA WA 1 2 3Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,na kufanya uinjilisti kati ya washiriki wa makanisa ya uongo.www.ACFAR.org barua pepe info@ACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664

Mafundisho ya Kibiblia kuhusu UtatuMungu ni mmoja mkamilifu kabisa akiwa na asili moja na nafsi tatu.Asili yake ni vile alivyo katika uhusiano wake na ulimwengu, yaani,vitu vyote alivyoumba. Nafsi zake ni tatu, zikiwa zinahusiana kati yao.Baba ni Mungu:Wakristo wanaposema kwambawanamwamini Mungu mmojakatika nafsi tatu (yaani, Utatu),hawamaanishi kwamba:Ni Mungu 1 katika miungu 3, au “Nawatakieni neema na amani kutokakwa Mungu Baba yetu na Bwana wetuYesu Kristo.” (1 Korintho 1:3; 8:6;Waefeso 4:4–6)Ni nafsi 3 katika nafsi moja, auMwana ni Mungu:Ni nafsi 3 katika miungu mitatu, au “Neno alikuwa Mungu.” (Yohane 1:1–5,14) Yesu anatambulika kama “Neno.”Ni nafsi 1 katika miungu mitatu. “Mimi na Baba, tu mmoja.” (Yohane10:30–33)Bali, wanamaanisha kwamba:Ni Mungu mmoja katika nafsi tatu.Kwa hiyo,Baba ni Mungu—nafsi ya kwanza yaUtatu.Mwana ni Mungu—nafsi ya pili yaUtatu.Roho Mtakatifu ni Mungu—nafsi ya tatuya Utatu.Kwa nini Wakristo wanauaminiUtatu?Biblia hufundisha wazi kwamba kunaMungu mmoja tu, ingawa nafsi zote zaMungu zinaitwa Mungu.Kuna Mungu mmoja tu: “Basi sikilizeni enyi Waisraeli! MwenyeziMungu, Mungu wetu, ni MwenyeziMungu mmoja.” (Kumbukumbu 6:4) “Kabla yangu hajapata kuwapo mungumwingine, wala hatakuwapo mungumwingine.” (Isaya 43:10; 44:6, 8; 45:5a) Tomasi, aliye mwanafunzi wa Yesu,alimwita Yesu, “Bwana wangu naMungu wangu.” (Yohane 20:28) Yesuhakumwambia Tomasi kwamba alikoseakwa kumwita hivyo, bali alikubalikukubali kuitwa hivyo. Wengine katikaMaandiko (k.m. Paulo na Barnaba, Matendo14), walikataa kuabudiwa kama miungu. “Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema:“Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumumilele na milele! Wewe wawatawala watuwako kwa haki.” (Waebrania 1:6–8). “Kwa sababu hiyo Mungu alimkwezajuu kabisa, akampa jina lililo kuu kulikomajina yote. Ili kwa heshima ya jina la Yesu,viumbe vyote mbinguni, duniani na kuzimuvipige magoti mbele yake, na kila mtu akirikwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufuwa Mungu Baba.” (Wafilipi 2:9–11)Paulo, mwandishi wa barua kwa Wafilipi,alisema kuhusu Yesu kilichosemwakuhusu Mwenyezi-Mungu katika Isaya45:23, halafu akamaliza kwa kusemaYesu ni Bwana, yaani, ni Mwenyezi-UKURASA WA 1 2

Mafundisho ya Kibiblia kuhusu UtatuMungu yuleyule wa Agano la Kale.Angalia aya hizi kuhusu umungu wa Yesu: Isaya7:14; Isaya 9:6; Yohane 1:1; Yohane 8:58, 59; Yohane10:30; Matendo 20:28; Waroma 9:5, 10:9–13;Wakolosai 1:15, 16; Wakolosai 2:9; Tito 2:13;Waebrania 1:3, 8; 2 Petro 1:1; 1 Yohane 5:20.Roho Mtakatifu ni Mungu: “Basi, Petro akamwuliza, “Anania,mbona Shetani ameuingia moyo wako nakukufanya umdanganye Roho Mtakatifu. . Hukumdanganya mtu; umemdanganyaMungu!” (Matendo 5:3–4) Mstari huuunamtambua Roho Mtakatifu kuwa Mungu. “Hapa Bwana ni Roho.” (2 Wakorintho3:17) Neno “Bwana” hapa lamrejeaMwenyezi-Mungu katika mstari waAgano la Kale (Kutoka 34:34) ambaoalinukuu katika mstari uliotangulia (2Wakorintho 3:16).Zaidi ya mistari 60 ya Biblia hutajanafsi tatu za Mungu pamoja: Mathayo 3:16–17 Mara tu Yesualipokwisha batizwa, alitoka majini; nakumbe mbingu zikafunguka, akaonaRoho wa Mungu akishuka kama njiwa nakutua juu yake. Sauti kutoka mbinguniikasema, “’Huyu ndiye Mwanangumpendwa, nimependezwa naye.’” 2 Wakorintho 13:14 “Neema ya Bwana YesuKristo na upendo wa Mungu na umoja waRoho Mtakatifu, viwe nanyi nyote.” Waefeso 4:4–6 “Kuna mwili mmoja naRoho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwana Mungu moja. Kuna Bwana mmoja,imani moja na ubatizo mmoja; kunaMungu mmoja na Baba wa wote, afanyakazi katika yote na yuko katika yote.” Tito 3:4–6 “Lakini wakati wema naupendo wa Mungu, Mwokozi wetuulipofunuliwa, alituokoa si kwa sababuya jambo lolote jema tulilotenda sisi, balikwa sababu ya huruma yake, kwa njiaya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliweupya na kuwa na maisha mapya kwakutuosha kwa maji. Mungu alitumiminiaRoho Mtakatifu bila kipimo kwa njia yaYesu Kristo ”Angalia pia Yohane 3:34–35; Yohane 14:26; Yohane15:26; Yohane 16:13–15; Waroma 14:17–18; Waroma15:13–17; Waroma 15:30; 1 Wakorintho 6:11, 17–19;1 Wakorintho 12:4–6; 2 Wakorintho 1:21, 22; 2Wakorintho 3:4–6; Wagalatia 2:21–3:2; Wagalatia4:6; Waefeso 2:18; Waefeso 3:11–17; Waefeso5:18–20; Wakolosai 1:6–8; 1 Wathesalonike 1:1–5;1 Wathesalonike 4:2, 8; 1 Wathesalonike 5:18–19;2 Wathesalonike 3:5; Waebrania 9:14; 1 Petro 1:2; 1Yohane 3:23–24; 1 Yohane 4:13–14; na Yuda 20–21.Haya yameandaliwa kutokana na The Trinity (RosePublishing, 1999) Mathayo 28:19 “Nendeni basi,mkawafanye watu wa mataifa yote wawewanafunzi wangu, mkiwabatiza kwajina la Baba, na la Mwana, na la RohoMtakatifu . . .”UKURASA WA 1 2Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,na kufanya uinjilisti kati ya washiriki wa makanisa ya uongo.www.ACFAR.org barua pepe info@ACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664

Aina Sita za Mafundisho ya UongoTabia za Mafundisho ya Makanisa ya UongoSi kwamba makanisa yote ya uongo yanafanya makosa yaleyale, lakini kuna sehemu kadhaa katika imani yetu ambazomara kwa mara zinachafuliwa na walimu wa uongo. Vipengele vifuatavyo vinadhihirisha sehemu sita za imani ambazomara kwa mara zinapotoshwa na walimu wa uongo, na vinaonyesha mifano mifupi ya jinsi wanavyouharibu ukweli.1 Ufunuo—Mara nyingi, makanisa ya uongoyatumia mafundisho ambayo huyapindisha,huyakana, na huyaongezea Maandiko kwa njiainayowaelekeza watu mpaka kwenye maangamizi.Wanadai kwa uongo kuwa na mamlaka ya kiutumeau kinabii. Mifano: Umormoni (Joseph Smith alijidai kuwa nabii;alitunga Kitabu cha Mormoni na “maandiko”mengine ya kimormoni.) M ashahidi wa Yehova (wadai kwamba Munguhuongea kupitia shirika la Mnara wa Mlinzi tu nakwamba ni watu wa “tabaka ya wapakwa mafuta”ambao wanaweza kufasiri Biblia.) K anisa la Waadventista Wasabato (HumwonaEllen G. White kama nabii maalumu wa Mungukatika siku za mwisho.)2 Mungu—Mara nyingi mafundisho yaohusisitiza miungu ya uongo au kugeuza kwa hatarimafundisho kuhusu Mungu wa kweli yawe ya uongo.Mifano: Umormoni (Hudai kwamba kuna miungu mingi,kwamba Mungu Baba aliwahi kuwa mtu aliyetendadhambi katika sayari nyingine, na kwamba sisitunaweza kufanywa kuwa miungu kama alivyoMungu Baba.) Mashahidi wa Yehova (Hudai kwamba Utatuwa Mungu ni uongo, wakisema kwamba MunguBaba tu ni Mungu wa kweli.) Wapentekosti wa Umoja wa Mungu Tu(Hudai kwamba Utatu ni uongo, wakisema Yesu niBaba, Mwana, na Roho Mtakatifu.)3 Kristo—Mara nyingi makanisa ya uongohukana kwamba Kristo ni Bwana, au ni binadamu,au ukweli wa kwamba yeye ni nani. Mifano: M ashahidi wa Yehova (Hudai kwamba YesuKristo alikuwa kwanza malaika Mikaeli, halafuakawa binadamu mkamilifu, na si Mungumwanadamu.) U mormoni (Hudai kwamba Yesu hakuzaliwa nabikira, kwa kuwa Mungu Baba alifanya tendo la ndoana Maria ili Yesu apate mwili wa kibinadamu.) Wakristadelfiani (Hudai Yesu hakuwaMungu. Alikuwa na asili ya dhambi, na alihitajikujiokoa kwanza kabla hajaweza kumwokoa mtuyeyote mwingine.)4 Wokovu—Makanisa ya Uongo mengihufundisha kuokolewa kunapatikana kupitia kutiimasharti mengi, au hudai wokovu ni nafasi yakuridhisha tamaa zetu. Hukana maana ya injili yakifo na ufufuo wa Yesu, nk. Mifano: Umormoni (Masharti yao ni pamoja na kujipatiawokovu kwa kuustahili kulingana na juhudi zetu nakuamini Joseph Smith ni nabii wa Mungu.) Mashahidi wa Yehova (Masharti yao ni pamojana kutumikia katika shirika la Yehova lilio lake lakweli, yaani shirika la Mnara wa Mlinzi.)5 Kanisa—Makanisa ya uongo hufanya juhudiza kuwatoa watu kutoka katika ushirikiano waWakristo wa kweli, mara nyingi hulikataa kabisakanisa. Mifano: Umormoni (Hudai kwamba makanisa yotemengine ni ya uongo na kwamba mafundisho yamakanisa yote mengine ni chukizo kwa Mungu.) Kanisa la Laodisia (Hadai kwamba Wakristowa kweli wote lazima watoke makanisa yao iliwamfuate William Branham, nabii wa kweli waMungu katika siku za mwisho.)6 Siku za Mwisho—Makanisa ya uongo maranyingi hujaribu kutabiri mambo ya mbeleni yakidaimamlaka kutoka kwa Mungu, kudai kuhusu kurudikwake Kristo kulishatendeka, nk. Mifano: Mashahidi wa Yehova (Walikosea kwenyekutabiri siku ya kurudi kwa Yesu kuwa katikamwaka 1874 halafu tena katika mwaka 1914. Piawalikosea kwenye kutabiri vita vya Armagedoni(yaani vita ya mwisho wa dunia kabla ya kujakwake Yesu) kuanza katika 1941 na 1975.Haya yameandaliwa kutokana na study na Robert M.Bowman, Jr.

Maonyo ya Maandiko dhidi ya Uchawina UshirikinaKatika Agano la Kale na AganoJipya, Mungu huwaamuru watuwake kuepukana na uchawi naushirikina, na huyatumia manenomakali. Kila wakati, Biblia huhusishauchawi na ushirikina na tendo lakuabudu sanamu, udanganyifu,hofu, ubatili, unajisi, na uasi. Munguhuona mambo haya kuwa maovu, yakishetani, na ya kustahili hukumu kalina ya haraka.Biblia Huhukumu Uganga naUaguziMwanzo 41:8, 242 Nyakati 33:6Isaya 47:9Yeremia 27:9–10Mika 5:12Nahumu 3:4Matendo 8:9–11; 19:19Wagalatia 5:19–21Ufunuo 9:21, 18:23, 21:8, 22:15Biblia Huhukumu KupigiwaRamli au Kujaribu Kuwasiliana naMizimuKumbukumbu 18:10–11Walawi 19:261 Samueli 28:3, 9Kumbukumbu 18:102 Wafalme 21:6, 23:242 Wafalme 17:17; 21:61 Nyakati 10:132 Nyakati 33:61 Nyakati 33:6Isaya 47:9, 12Isaya 8:19, 19:3Yeremia 27:9Matendo 8:9–11, 18–21; 13:6–12; 19:19Ufunuo 9:20, 21; 18:23, 21:8; 22:15Biblia Huhukumu Matumizi yaHiriziIsaya 3:18–20Ezekieli 13:18–20Yeremia 27:9Biblia Huhukumu KulogaKumbukumbu 18:9–11Isaya 47:9, 12Mika 5:12Biblia Huhukumu Kupiga BaoBiblia Huhukumu UchawiWalawi 19:262 Wafalme 17:17, 21:6Walawi 19:31, 20:6Kutoka 7:11, 22; 8:7, 18–19Kutoka 22:18Kumbukumbu 18:10, 14Walawi 19:26Kumbukumbu 18:10, 141 Samueli 15:23UKURASA WA 1 2Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,na kufanya uinjilisti kati ya washiriki wa makanisa ya uongo.www.ACFAR.org barua pepe info@ACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664

Maonyo ya Maandiko dhidi ya Uchawina UshirikinaNini KinachofanyaUnajimuUkubalike?2 Wafalme 17:17, 21:62 Nyakati 33:6Isaya 2:6Yeremia 27:9–10Matendo 16:16–20Biblia Huhukumu UshirikinaKumbukumbu 18:10, 141 Samueli 15:232 Wafalme 21:6Mtetezi wa imani waKikristo aitwaye VishalMangalwadi, katika kitabu chakeWisdom from India: Astrology (HekimaKutoka Uhindi: Unajimu), anaainishasababu tatu kuu zinazofanya unajimukuwavutia watu wengi siku hizi:2 Nyakati 33:6 Unajimu humpa mtu jibu lamatatizo yake.Mika 5:12Nahumu 3:3–4 Unajimu huondoa kujihisikuwa na hatia na adhabu.Wagalatia 5:19–21Biblia Huhukumu Unajimu(Kubashiri kwa Kuangalia Nyota)Kwa kuwa unajimu ni namna yakubashiri mambo yajayo, ni marufukukufanya hivyo kulingana na aya kamaWalawi 19:26. Pia tunaweza kujifunzazaidi tukiangalia mistari kama ifuatayo: Isaya 47:13–15 (hapo wanajimuwalidharauliwa na kuhukumiwa) Unajimu humpa mtumwongozo wakati anapohisikukata tamaa na kupotezamwelekeo.Unajimu Unafanya Kazi Vipi?Unajimu si tu kwamba unakatazwa kwenyeBiblia, bali pia unajimu ni jambo la kishetani. Yeremia 8:1, 2: 10:2 (wale wanaofuatajua, mwezi, na nyota, na kuviabudu, nakutafuta ushauri huhukumiwa.)Mwandishi mmoja wa kitabu kinachohusu Daniel sura ya 2, 4, 5 (Baada yawanajimu na wapiga bao kudai kwambakufasiri ndoto za Nebukadneza namaono ya Belshaza hakuwezekani,Danieli alivifasiri kwa msaada waMungu.)aliwahi kuwa mnajimu mahiri, alieleza,Haya yameandaliwa kutokana na Christianity, Cults,and the Occult (Rose Publishing, 2006)unajimu, Charles Strohmer, What YourHoroscope Doesn’t Tell You, ambaye pia“Wafuasi wa unajimu wanawasiliana—bila wao kujua—na watu wa kiroho waudanganyifu wenye ufahamu fulani.”Anaendelea kueleza kuwa wanatumiajedwali au chati ya kinajimu kama chombocha kuwasiliana na hizo roho kwa ajili yakujigundua binafsi kwa njia ya unajimu.UKURASA WA 1 2

Namna 10 za Kufanya Uinjilisti kati yaWashiriki wa Makanisa ya Uongo1 Fahamu mafundisho ya msingi ya Biblia. Hakuna mtu yeyote ambaye anawezakujua kila fundisho la uongo la kila kanisa la uongo, lakini Wakristo wajuao Bibliavizuri wanaweza kukuza uwezo wao wa kutambua mafundisho yasiyo sahihi. Ujue kileunachokiamini na kwa nini unakiamini hivyo.2 Usitegemee kwamba kila mshiriki wa kanisa la uongo anaamini sawa.Wafuasi wa kundi moja wanaweza kutofautiana kwa kiasi cha kuelewa kwao (au kwamaoni yao). Muulize mtu huyo kuhusu imani yake binafsi; usimshtaki.3 Mara nyingi washi

www.ACFAR.org barua pepe infoACFAR.org simu 256782 000 664 ofisi 256713 000 664 Tunawatayarisha watu wa Mungu kwa ajili ya kupambanua, kutetea imani,